Tuesday, June 26, 2012

URUSI, HISPANIA ZAWEKWA KIKAANGONI KUFUATIA TUHUMA ZA UBAGUZI.

SHIRIKISHO la soka barani Ulaya-UEFA imezifungulia mashtaka vyama vya soka vya Hispania na Urusi kutokana na matukio ya kibaguzi yaliyoonyeshwa na mashabiki wa timu zao za taifa katika michuano ya Ulaya inayoendelea nchini, Poland na Ukraine. Mashtaka hayo yamekuja kufuatia taarifa kuwa kulikuwa na baadhi ya mashabiki Hispania wakipiga kelele za nyani kumlenga mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli huku mashabiki wa Urusi wakiwa wamemlenga beki wa Jamhuri ya Czech Theodor Gebre Selassie katika michezo ambayo timu hizo zilikutana. Shirikisho hilo limesema kuwa limefungua kesi za utovu wa nidhamu zilizoonyeshwa na mashabiki hao ambapo bodi ya kupambana na uaguzi katika mchezo wa soka barani Ulaya itakutana Alhamisi kushughulikia suala hilo.

No comments:

Post a Comment