Friday, June 8, 2012

UHOLANZI YAKUMBWA NA SUALA LA UBAGUZI KWA WACHEZAJI WAKE WEUSI.

MSEMAJI wa timu ya taifa ya Uholanzi amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo walikuwa wakisikia kelele za mashabiki wakishangilia kwa kelele za nyani wakiwalenga baadhi ya wachezaji weusi waliopo katika timu hiyo katika Uwanja wa Wisla Krakow walipokuwa wakifanya mazoezi jana. Kocha wa timu hiyo Bert van Marwijk, maofisa wa kikosi hicho pamoja na waandishi wa habari waliokuwa wakishuhudia mazoezi ya timu hiyo hawakusikia kelele zozote za kibaguzi wakati wa mazoezi ya timu hiyo Jumatano lakini nahodha wa kikosi hicho Mark van Bommel amesema kuwa yeye pamoja na wachezaji wenzake walisikia kelele hizo. Msemaji huyo amesema kuwa wachezaji walisikia kelele hizo ambazo zilikuwa zikipigwa na mashabiki wapatao 30,000 waliomiminika kushuhudia mazoezi ya timu hiyo ndio maana wakahama upande mwingine wa uwanja kwa ajili ya kuendelea na mazoezi yao. Hatahivyo Shirikisho la Soka la nchi hiyo limesema kuwa halitafungua mashitaka kuhusiana na suala hilo kwa Shirikisho la Soka Ulaya-UEFA kutokana na kelele hizo kuchanganyika na mambo ya kisiasa inayozikabili nchi hizo. Uholanzi ambao walishika nafasi ya pili katika michuano ya kombe la Dunia mwaka 2010 wanatarajiwa kuanza mchezo wa kwanza wa michuano ya Ulaya katika kundi B dhidi ya Denmark mchezo ambao utachezwa Kharkiv, Ukraine kesho.

No comments:

Post a Comment