Monday, June 25, 2012

UEFA YATANGAZA WAAMUZI WA NUSU FAINALI EURO 2012.

Cuneyt Cakir
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limetangaza majina ya waamuzi watakaochezesha michezo ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya itakayochezwa Jumatano na Alhamisi ya wiki hii. Mwamuzi Cuneyt Cakir kutoka Uturuki ndio anatarajiwa kuchezesha mchezo kati ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo Hispania dhidi ya Ureno mchezo ambao unatarajiwa kupigwa jijini Donetsk, Ukraine kesho kutwa. Wakati Stephane Lannoy kutoka Ufaransa yeye atachezesha mchezo baina ya Ujerumani ambao watakuwa wakijaribu kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya kushindwa kutamba mbele ya Hispania mwaka 2008 dhidi ya Italia mchezo utakaochezwa jijini Warsaw, Poland. Italia wametinga hatua hiyo baada ya kuwaondoa kwa changamoto ya mikwaju ya penati Uingereza baada ya timu hizo kushindwa kufungana katika muda wa kawaida wakati Ujrumani wao waliingia kwa kishindo katika hatua hiyo baada ya kuifunga Jamhuri ya Czech mabao 4-2.

No comments:

Post a Comment