Sunday, June 24, 2012

UEFA YASHTUSHWA NA MAAMUZI YA CAS.


 

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limeshangazwa na kusikitishwa na maamuzi ya Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS kwa kuiruhusu klabu ya Bursaspor ya nchini Uturuki kushiriki michuano ya Ligi ya Ulaya au Europa League. UEFA iliifungia klabu hiyo mwaka 2010 kushiriki michuano yoyote ya Ulaya kwa mwaka mmoja kutokana na kushindwa kulipa ada ya uhamisho mwaka 2007. Mbali na kuiondolea adhabu klabu hiyo CAS pia imeongeza faini ambayo UEFA iliitoza klabu hiyo kutoka paundi 50,000 mpaka kufikia kiasi cha paundi 250,000. Klabu hiyo ilimaliza katika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo msimu uliopita lakini walifanikiwa kupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo ya Ulaya baada ya kushinda katika michezo ya mtoano.

No comments:

Post a Comment