Thursday, June 7, 2012

TANZANIA SOCIAL NEWS: RAIS WA AWAMU YA TATU TANZANIA ATOA KITOWEO KWA CONGREGATION OF THE HOLY GHOST


RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa ametoa zawadi ya ng'ombe wawili wenye thamani ya zaidi ya ShMilioni 1.4 kwa ajili ya kitoweo cha wajumbe 15 kutoka nchi 60 duniani ambao watashiriki Mkutano wa Dunia wa Shirika la Roho Mtakatifu (Congregation of the Holy Ghosty), unaotarajiwa kuanza Juni 24 mjini Bagamoyo.

Akizungumza shambani kwake eneo la Vikawe, Bagamoyo mkoa wa Pwani mara baada ya kukabidhi ng'ombe hao kwa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ambayo inaongozwa na Padri Joseph Shio, Rais huyo mstaaafu alisema ameguswa kutoa msaada huo kutokana na kulelewa na wamisionari wa shirika hilo.


Amesema Rais huyo mstaafu kuwa licha ya yeye pia kuna wanafunzi wengine ambao walipita Pugu Sekondari ambao nao wamejitolea walicho nacho kuhakikisha mkutano huo wa kwanza kufanyika barani Afrika unafanikiwa.

Mkapa amesema kuwa ng'ombe hao wawili ambao ametoa ni shemu ya zawadi ambazo alipewa na watanzania wakati anastaafu hivyo haoni kwanini asiwatoe zawadi kwa ajili ya shughuli hhiyo.

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, mkuu wa shirika hilo Padri Shio alisema Rais Jakaya Mrisho Kikwete ndie ambaye ataufungua rasmi mkutano huo wa mwezi mmoja hapo Juni 29 mwaka huu.

Amesema mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili lilipotoka shirika, lilipo na litakapokwenda sanjari na changamoto ambazo zinalikabili na kutengeneza dira ya miaka nane hadi 10 ijayo.

Mkuu huyo amesema watendaji wakuu wa shirika hilo wangeweza kuufanya mkutano huo popote lakini wameona umuhimu wa Tanzania na historia ya mji wa Bagamoyo ambako ndipo shirika hilo lilipoingilia mwaka 1868.

Amesema shirika hilo linatambulika kutoka na jitihada zake za kupiga vita biashara ya utumwa wakati huo kwa kuwanunua na kuwapatia elimu na matibabu wahanga wa biashara hiyo na toka wakati huo shirika hilo limezidi kupanuka nchini na duniani kwa ujuma likitoa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya na masuala ya uchumi.

No comments:

Post a Comment