Saturday, June 16, 2012

TANZANIA SOCIAL NEWS: KORTINI KWA KULIMA BHANGI


Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma  limemkamata mtu mmoja, aliyefahamika kwa jina la Mwanga Msemakweli(41), Mkulima, Mkazi wa Ising’ht kwa tuhuma za kulima Bhangi katika shamba lake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen alisema tukio hilo lililotokea tarehe 14/06/2012 majira ya saa 09:00 asubuhi katika kijiji cha Insig’ht Wilaya ya Mpwapwa Mkoni Dodoma, baada ya Jeshi la Polisi  kupitia Mkakati wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kupokea taarifa toka kwa wanakijiji wema kuwa kuna mtu analima bangi katika shamba lake.

Zelothe Stephen alisema iliwashangaza wanakijiji na wakulima wenzake kuona wao wamevuna mazao yao katika mashamba yao lakini mwenzao alikuwa hajavuna, hivyo kumtilia shaka na kumfuatilia na hatimaye kutoa taarifa Polisi ambao walikwenda kumkamata.

Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hizo, walijipanga na  kwenda kumkamata mtuhumiwa na kisha kumpekua nyumbani kwake na   kumkuta na  kete kumi na tisa za bangi pamoja na  bangi iliyokuwa haijasokotwa ikiwa kwenye mfuko wa Nailon ambapo ilipopimwa ilikutwa ni gram mia tano.

Aidha Zelothe amesema Jeshi la Polisi Wilayani Mpwawa kwa kushirikiana na wanakijiji cha insig’ht Walifanikiwa kuliteketeza kwa moto shamba hilo la bangi lenye ukubwa wa hekali mbili.

Kamanda Zelothe Stephen ametoa wito kwa wakulima kuacha kulima zao hilo la bangi kwani ni kinyume na sheria za nchi  na kuahidi kwamba mkulima yeyote atakayegundulika kulima zao hilo, hatua kali na za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Imeandikwa na Luppy Kung’alo, Dodoma

No comments:

Post a Comment