Tuesday, June 19, 2012

TANZANIA RELIGIOUS NEWS: WACHUNGAJI 2000 KUKUTANA ARUSHA KUIOMBEA TANZANIA


Viongozi 2000 wa makanisa mbalimbali kutoka katika nchi 5 wanatarajia kukutana jijini Arusha na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia za nchi,pamoja na mapigano ya kidini yalioibuka Zanzibar

Askofu wa makanisa ya Intenational Evangelism Centre ya hapa nchini Eliud Isangya (pichani) alisema hayo wakati akifanya mahojiano na libeneke la kaskazini ofisini kwake ambapo alisema kuwa viongozi hao watakutana jijini hapa wiki ijayo.


"Kwa sasa zipo changamoto kubwa sana ikiwemo changamoto ya mabadiliko ya tabia za nchi ambayo inawaasumbua wananchi wengi sana hasa wa vijijini lakini kama taasisi mbalimbali zikiwemo za dini zitawahamasisha hata waumini wake ni wazi kuwa jamii haitaweza kukumbwa na baa la ukame kwa maana hiyo tutajadili masuala kama hayo ambayo yanazitesa jamii za watanzania walio wengi."

Aidha alibainisha kuwa wanasayansi wanabuni vitu vipya na vina uwezo wa kuwasaidia jamii kwanini sisi kama wadau wa nchi hii tusiwe wabunifu wa kusadia hata kuombea taifa katika majanga mbalimbali ambayo ni kikwazo cha maendeleo,tunataka tufanye hivyo ili kurudisha hata vitu ambavyo vimepotea kwenye nchi hii ya Tanzania

Mbali na hayo Eliud amezitaka Taasisi nyingine za dini kuhakikisha kuwa kila mara zinayafanyia maombi changamoto ambazo zipo kwenye jamii kwa kuwa wao ndio wana nafasi kubwa sana ya kuweza kulikomboa taifa la Tanzania

No comments:

Post a Comment