Friday, June 15, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: UCHAGUZI WA VIONGOZI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB (YANGA) KUJAZA NAFASI ZILIZO WAZI


K
amati ya Uchaguzi ya TFF inawataarifu wadau na wapenzi wa soka kuwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa YANGA kujaza nafasi zilizowazi za Kamati ya Utendaji unaendelea vizuri chini ya Kamati ya Uchaguzi ya YANGA.


Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea kutoka Kamati ya Uchaguzi ya YANGA nakala za fomu za maombi ya uongozi wa YANGA pamoja na nakala za vyeti vya elimu vya waombaji uongozi kama sehemu ya taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi huo wa YANGA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa baadhi ya waombaji uongozi wamewasilisha nakala za vyeti vya kuhudhuria masomo ya sekondari (Secondary School Leaving Certificate) badala ya nakala za vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya sekondari (Certificate of Secondary Education).

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekwisha ielekeza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kuwataka wagombea wote kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10(4) na (5) inayowataka wagombea wote kujaza Fomu Na.1 ya maombi ya uongozi na kuambatanisha nakala ya cheti cha Elimu ya Sekondari (Certificate of Secondary Education) kama ilivyoainishwa kwenye Fomu Na.1 kipengere Na.9. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA iwashauri wagombea ambao vyeti vyao vimepotea wawasiliane na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa maandishi ili kupata ‘Statement of Examination Results’itakayotumwa kwa Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kupitia TFF kuthibitisha kuwa wamehitimu elimu ya kidato cha nne.

Uhakiki wa vyeti vya elimu ya sekondari vya waombaji uongozi hufanywa na NECTA na vyuo husika kwa elimu ya juu kwa chaguzi za wanachama wa TFF. Wanachama wote wa TFF wanatakiwa kuzingatia kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi.
 
Imetolewa na:
IDARA YA HABARI
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment