Thursday, June 14, 2012

TANZANIA ENTERTAINMENT NEWS: DIAMOND AONGOZA KWA WASANII WA BONGO FLEVA KWA MAPATO


K
UFUATIA mafanikio alinayoyapata hivi sasa kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya Bongo, staa wa muziki huo Naseeb Abdul ‘Diamond’ ndiye mkali anayeingiza mkwanja mrefu zaidi kuliko nyota wote wanaotamba hivi sasa hapa nchini.

Uchunguzi umebaini kuwa Diamond anaingiza kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 16 kwa kila shoo mbili anazofanya akiwa ndani na nje ya jiji la Bongo.
Katika kuhakikisha kuwa ukweli unapatikana mpekuzi ilimsaka Diamond na baada ya kufanikiwa kumpata alikiri kufikia kiwango hicho .

“Nashukuru Mungu kwa kufika hapa na ukweli ni kuwa nalipwa mkwanja huo na hii imekuja kufuatia kuweka nguvu zangu katika muziki na kufanya vitu vizuri kwa kuwa gemu ndiyo maisha yangu” alisema Diamond.

Akiendelea zaidi nyota huyo wa ‘Songi’ la ‘Mawazo’ alianika kuwa mafanikko haya yanakuja pia kutokana na sapoti anayoipata kutoka kwa watu wake wa karibu akiwemo Mama yake mzazi na wengine kibao.

No comments:

Post a Comment