Tuesday, June 19, 2012

MBEYA UPDATE: WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WATAKIWA KUONGEZA BIDII


WANAFUNZI wa Shule za Msingi nchini Tanzania wametakiwa kuongeza juhudi katika masomo yao licha ya changamoto wanazokutana nazo wanapokuwa mashuleni.
Akizungumza na Redio Mbeya FM, Mkuu wa Shule ya Msingi Mwasote Jijini Mbeya Yuda Mwakisu amesema upungufu wa vitabu vya masomo mbalimbali ikiwemo Hisabati husababisha kiwango cha ufaulu kupungua.

Akitolea mfano wa Shule yake amesema mara baada ya kung’amua changamoto walizonazo watoto walikaa baina yao walimu na wazazi na kuungana kwa pamoja katika kuwasaidia watoto ili waweze kufaulu. Mwalimu Mwakisu amesema baada ya kungaana pamoja waliamua kuwa baada ya masomo yanayoisha saa za mchana wanafunzi wanatakiwa kurudi kwa muda wa ziada kuanzia saa 9-12 jioni.

Aidha amesema baada ya kutia bidii katika kuwafundisha wanafunzi hao na kwamba mwaka 2011 wanafunzi wa shule ya msingi Mwasote walifaulu  104 kati ya wanafunzi 122, wavulana 49 na wasichana 55.

Pia amewataka wazazi waachie watoto wasome na sio kuwafundisha mambo ya ajabu.

No comments:

Post a Comment