Tuesday, June 19, 2012

MBEYA UPDATE: WALEMAVU WATAKIWA KUTOFICHWA


W
AZAZI wenye watoto walemavu wametakiwa kutowaficha watoto hao kwani nao wana haki za msingi kama watoto wengine hapa duniani.

Katika mahojiano maalum na JAIZMELALEO Mwalimu Mkuu wa Child Support Tanzania James Omoding amesema wazazi wengi wamekuwa na tabia ya kuwaficha watoto wao pindi wanapoonekana kuwa na ulemavu.

Omoding amesema kuwaficha huko ni kuwanyima haki za msingi watoto hao kwani wana haki kama watoto waengine  katika  ulimwengu.

Pia kufuatia changamoto ya upungufu wa vitabu katika mashule kwa ajili ya watoto walemavu Serikali kwa upande wake imeatakiw akupungua kama sio kuondoa kabisa Kodi ya vifaa vya watoto hao ilikuwezesha elimu kwa walemavu.

No comments:

Post a Comment