Wednesday, June 20, 2012

MBEYA UPDATE: WAKULIMA WARUHUSIWA KUUZA KAHAWA MAHALI POPOTE


Mgogoro kati ya kampuni ya Lima na vikundi vya wakulima wa kahawa kuhusu ununuzi wa zao hilo wilaya ya Mbeya vijijini umemalizika baada baraza la madiwani la halmashauri kuruhusu wakulima kuuza zao hilo sehemu yoyote wanayoitaka.
Akisoma taarifa ya utafiti iliyofanywa hivi karibuni wilayani humo Mwenyekiti wa kamati maalumu iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia mgogoro huo Msuba Luoakisyo amesema wakulima wamekuwa wakilalamikia kushuka kwa bei ya zao hilo, ununuzi holela pamoja na wizi wa kahawa zikiwa mashambani.

Katika kikao hicho cha dharula madiwani waliafikiana kutoa uhuru wa soko kwa wakulima kuuza kahawa, na kwamba msimamo wa bei ya zao hilo ibaki kuwa chini ya wakulima wenyewe.

Akihitimisha kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya na diwani wa kata ya Andason Kabenga ametoa pongezi kwa madiwani hao kufikia muafaka wa suala hilo ambalo limekuwa likisumbua kwa kipindi kirefu.
Imeandikwa na Ezekiel Kamanga, Mbeya

No comments:

Post a Comment