Monday, June 11, 2012

MBEYA UPDATE: WAKULIMA WAONYWA

W
AKULIMA Mkoani Mbeya wameonywa  kutofanya ubadhirifu wa chakula kwa kuwa mwaka huu kutakuwa na njaa kali tofauti na mwaka jana.
Akizungumza katika mahojiano na Blogu ya JAIZMELALEO katika kijiji cha Lusungo Wilayani Mbeya Vijijini Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Sadick Kamwela amesema mwaka huu kutakuwa na njaa kutokana na uchache wa mazao waliyoyapata.

Kamwela amesema licha ya wakulima wengi kujitahidi kulima kwa wingi mazao lakini Mvua ilisababisha mazao hayo yasitoe mazao mengi kwa kuwa ilikatika wakati mazao yakiwa bado hayajakomaa vizuri hivyo kusababisha walima kupata mazao kidogo.

Kutokana na upungufu wa chakula Kamwela alitoa rai kwa wakulima kupunguza matumizi mabaya ya chakula kwa kuuza bila mpangilio kwa ajili ya hanasa na pombe wakati wanatambua kuwa mavuno ya mwaka huu hayatokidhi mahitaji yao.

Aidha Kamwela ameiomba Serikali kupitia mawakala wanaosambaza mbolea na mbegu zapembejeo kusambaza  wakati wa mavuno badala ya kusambaza miezi ambayo wakilima wengi wanakuwa wameshatumia vibaya mazao yao hivyo kushindwa kumudu gharama za kununulia vitu hivyo muhimu.

Naye Mkulima wa kijiji hicho ambaye pia ni mwalimu wa kikundi cha Wekeza Upate Pembejeo (WEUPE) Ednah Mwatujobe amesema kuwa nivyema wakulima wakatimia mbegu ambazo zinastahimili ukame kwa kuwa  Mvua za siku hizi hazitabiliki.

Amesema kuwa baadhi ya wakulima wenzao wameshindwa kabisa kupata mazao kutokana na kupanda mbegu ambazo hazikuweza kustahimili ukame licha ya kuwahi kupanda mbaegu hizo mapema kuliko wao lakini wao wamepata mazao kiasi kizuri kutokana na mbegu walizopanda aina ya Tan250, Tan254 na Tan H600 za kampuni ya Tanseed International Ltd.

 Ameongoza kusema mbegu hizo zimekuwa msaada mkubwa katika bonde la Songwe kutokana na kuendana na udongo pia kuvumilia ukame jambo ambalo alisema wamenufaika nazo licha ya kuchelewa kupanda kama walivyowahi wenzao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mtenda Kyela Rice amejitolea kwa kuwalipia gharama zote wakulima kutoka kikundi cha WEUPE ili waende kujifunza mambo ya kilimo katika maonyesho ya nane nane yatakayofanyikia kitaifa Mjini Dodoma mwaka huu.

No comments:

Post a Comment