Thursday, June 14, 2012

MBEYA UPDATE: GOBOLE LAMLAZA MAHABUSU


M
kazi mmoja wa Kijiji cha Mbangala,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,Bwana Issah Malala(32) anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukutwa na silaha aina ya gobole nyumbani kwake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Diwani Athuman,amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa majira ya saa 3:00 usiku,Juni 11 mwaka huu na kwamba alikuwa anamiliki silaha hiyo kinyume cha sheria.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa bado anashikiliwa na jeshi lake na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili kujibu shtaka la kumiliki silaha hiyo bila kibali.

No comments:

Post a Comment