Wednesday, June 13, 2012

MBEYA UPDATE: CHADEMA KUTUMIA NGUVU YA UMMA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka serikali iendelee kusimamia miradi ya maendeleo vizuri la sivyo nguvu ya umma itatumika.
 BENSON KAGAIRA


Akizungumza katika siku ya mwisho ya Mafunzo kwa Madiwani na Viongozi wa chama hicho Nyanda za Kusini Mkurugenzi wa Oganaizesheni ya Mafunzo Singo Benson Kagaira amesema suala la usimamizi wa masuala ya kimaendeleo ni la serikali na sio chama hicho kwa sasa isipokuwa kwa madiwa wa chama hicho waliopo madarakani.

Kagaira amesema madiwani hao kutoka mikoa ya Ruvuma, Mbeya Iringa na Rukwa wameeleza changamoto zinazowakabili ikiwemo chama cha Mapinduzi kuzuia baadhi ya mambo yasieendelee kwa manufaa ya wananchi.

Mkutano huo wa ndani unamalizika leo jioni huku ikitarajiwa kutoka na maazimio ili kuendeleza harakati ya Movement for Change.

No comments:

Post a Comment