Friday, June 22, 2012

MBEYA UPDATE: AFA KWA KUGONGWA NA GARI


M
kazi wa Isyonje aliyefahamika kwa jina la Rasi Mkude (35) amefariki dunia Alhamisi baada ya kugongwa na gari maeneo ya Isyonje wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Mbeya imesema Mkude alifikwa na mauti hayo baada ya gari lililokuwa likiendeshwa na Dereva John Msika(40)  lenye namba za usajili T. 453 BDC aina ya Toyota Coaster kumgonga marehemu katika barabara ya Tukuyu-Mbeya wilayani humo majira ya 12 jioni.

Taarifa hiyo imeongeza kusema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi  na mtuhumiwa yupo mahabusu wakati upelelezi zaidi ukiendelea.

No comments:

Post a Comment