Wednesday, June 27, 2012

MBEYA UPDATE: ADONDOKA KWENYE GARI, AFA


M
tu anayefahamika kwa jina la Martine Ahobekile (56), amefariki dunia papo hapo baada ya kudondoka kutoka kwenye gari alilokuwa amepanda katika eneo la Uyole, jijini Mbeya.

Kamanda wa polisi na Kamishna Msaidizi wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, Taarifa kutoka polisi zinasema Martine Ahobokile mkazi wa Uyole Jijijni Mbeya alidondoka kutoka katika gari aina ya Land Rover ambalo halikujulikana kwa namba katika ajali iliyotokea eneo la Uyole, barabara ya Mbeya-Iringa jijini Mbeya. Pia taarifa kutoka polisi zinasema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika kwa jina wa makazi na alikimbia na gari mara tu baada ya kusababisha ajali. Aidha taarifa hizo zinasema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya na polisi bado wanaendelea na upelelezi.

No comments:

Post a Comment