Sunday, June 24, 2012

mama amuunguza mwanae kwa sigara

Julie Minter ameshindwa kabisa kuisamehe nafsi yake, baada ya tukio la mwaka 1998 la kuvuta sigara chumbani, na kuisahau na kusababisha moto kwenye chumba cha  mtoto wake  Terri  Calvesbert ambae alikua na miezi 22 wakati huo, na kumsababishia maumivu na majeraha makubwa.            

 
Julie Minter, alilazimika kuondoa na kukaa mbali na mtoto wake kwa sababu hawezi kujisamehe kwa kitendo alichofanya. Anadai hakuwahi kuvuta sigara chumbani, ila kwa mara ya kwanza amefanya hivyo, na tukio hilo la kuumiza limetokea. Julie aliachana na baba wa mtoto wake huyo miezi miwili kabla ya moto huo, ila waliamua kuishi pamoja kama marafiki tu.


Mtoto Terri kabla ya kuungua na moto. Julie ameeleza kwamba, usiku huo Terry alikua anasumbua kulala, akambembeleza bila mafanikio, akaamua kuwasha sigara  na kuvuta. Aliamua kutoka chumbani kwenda jikoni, akiacha sigara hiyo chumbani. Akiamini kuwa mtoto atalia, ila atanyamaza na kulala muda si mrefu. Ila alishangaa kusikia mtoto akizidi kulia kwa nguvu na alipoingia ndani alikuta moto mkubwa,asijue cha kufanya. ndipo alipoita zima moto, hata hivyo walipofika walikuta Terri ameshaungua sana. Waokoaji hao wamekiri hawajawahi kuona mtu aliyeungua sana kama huyo na bado akawa hai.


Terri anavyoonekana sasa, hata hivyo amesema hamalaumu mama yake kwa tukio lililotokea, ila anasikitika kwamba hajapata nafasi ya kumjua mama yake vizuri, alipata nafasi ya kumuona mara moja miaka minne iliyopita baada ya Julie kuitwa kwenye kikao, ila baada ya hapo hajawahi kumuona tena. yeye anaamini hakuna anaestahili lawama juu ya hili. Na alimtumia mama yake ujumbe kumwambia kuwa, hastahili kujilaumu juu ya hili, kwani yeye ni mama yake, na atabaki uwa mama yake siku zote 

Terri anaishi na baba yake Paul na mama yake wa kambo Nikki baada ya mama yake kuhama na kuamua kukaa mbali na watu wote, ikiwemo Terri hata wazazi wake. Mama huyo ameamua kuishi maisha kana kwamba hajawahi kua na mtoto, ili aweze kusahau machungu ya tukio hili. Terri kwa sasa ana miaka 15.
Picha na habari kutoka The Sun 

No comments:

Post a Comment