Monday, June 25, 2012

LEO KATIKA HISTORIA: LIBERIA YAPATIKANA


1812
Na siku kama ya leo miaka 190 iliyopita kundi la watumwa weusi wa Marekani ambao walikuwa wameachiwa huru na wamiliki wao wazungu lilirejea Afrika na kuweka makazi yao katika ardhi inayojulikana hii leo kwa jina la Liberia.
Raia weusi wa Marekani walianzisha mapambano tangu mwanzoni mwa karne ya 19 Miladia lengo likiwa ni kujiondoa katika utumwa wa wazungu na kuasisi nchi kwa ajili ya raia weusi. Rais wa kwanza wa Liberia alikuwa Joseph Jenkins Roberts ambaye alikuwa mtumwa kutoka jimbo la Virginia.

No comments:

Post a Comment