Tuesday, June 19, 2012

LEO KATIKA HISTORIA: KUWAIT ILIJIPATIA UHURU WAKE


Siku kama ya leo miaka 51 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 19 Juni 1961, Kuwait iliyoko katika eneo la Ghuba ya Uajemi ilijipatia uhuru wake baada ya kufutwa mkataba wa kikoloni uliosainiwa mwaka 1899 kati yake na Uingereza.
Silsila ya familia ya as Swabah iliasisiwa nchini humo katikati ya karne ya 18 na mwishoni mwa karne ya 19, Kuwait iliiomba Uingereza iihami katika kukabiliana na utawala wa Othmaniya. Ulipofika mwaka 1899, Uingereza na Kuwait zilifanya makubaliano ambayo yaliiweka Kuwait chini ya ukoloni wa Uingereza. Hata hivyo Uingereza ilitumia vibaya makubaliano hayo kwani ilianza kupora utajiri na maliasili ya eneo hilo na hasa mafuta.

No comments:

Post a Comment