Friday, June 22, 2012

LEO KATIKA HISTORIA: ADOLF HITLER ALIANZISHA VITA NYINGINE


1939
Siku kama ya leo miaka 71 iliyopita jeshi la Ujerumani ya Kinazi lilianza mashambulizi makubwa dhidi ya Urusi ya zamani kwa jina la Operesheni ya Barbarossa.
 
Kwa utaratihu huo Adolph Hitler alianzisha vita vingine katika upande wa mashariki mwa Umerumani kwa shabaha ya kutimiza mipango yake ya kutaka kujitanua zaidi. Hadi wakati huo dikteta huyo wa Ujerumani alikuwa tayari ameteka nchi kadhaa za Ulaya. 

Baada ya kushambulia Urusi, askari wa Ujerumani walisonga mbele ya kufika katika viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo, Moscow. Hata hivyo jeshi la Manazi wa Ujerumani lilipata matatizo makubwa baada ya kuanza kipindi cha baridi kali na kushindwa kusonga mbele. Wananchi na jeshi la Urusi katika miji mbalimbali ya nchi hiyo hususan Moscow, Leningrad na Stalingrad walipambana vikali na jeshi la Ujerumani na kulilazimisha kurudi nyuma. Mwezi Agosti 1944 jeshi la Urusi lilifika katika mipaka ya Ujerumani. Mashambulizi ya Ujerumani dhidi ya Urusi yalidhofisha utawala wa Hitler na hatimaye kushindwa kikamilifu.

No comments:

Post a Comment