Friday, June 22, 2012

KONA YA MWALIMU: NENO LA MCHUNGAJI MATTHEW SASALI LAWEZA KULETA IMPACT


Ulimwengu uko hivi ulivyo leo kwa sababu miaka fulani huko nyuma watu wamewahi kuwa wadadisi...ambao ulipelekea kuwa na mambo mengi mazuri na makubwa ya hivi leo.

Udadisi ni hali inayompelekea mtu kuwa "genius"mwenye ufahamu mkubwa. Sidhani kama unaweza kukuta mwna taaluma mkubwa bila nyuma yake kuwa na Tabia ya Udadisi...


Hebu tuangalie kwa nini Udadisi ni kitu cha thamani...
1....Hufanya ufahamu kujishughulisha...kutokuwa na fikra Mgando.
Watu wadadisi mara zote huuliza maswali na hutafuta tafuta majibu ya maswali hayo katika fikra zao.Ufahamu wao mara zote hujishughulisha,na kwa kadri hufahamu unavyojishughulisha ni kama misuri ya kufikiri na kupata majibu nayo hutanuka...na kwa sababu huwa tabia na zoezi la mara kwa mara...basi ule uwezo wa akili unaosababishwa na udadisi hufanyika imara na fikra hukuzwa.

2....Hufanya ufahamu wako kufungua milango ya mawazo mapya
Kumbuka pale unapoanza udadisi juu ya kitu fulani...fahamu zako huweka matarajio na kuwa tayari kupokea mawazo mapya ya jambo lile.
Na pindi wako linapokuja fahamu hulitambua na kulikubali.Bila udadisi wazo jipya laweza kukupita na kujikuta ukikosa mambo mengi kwa sababu tu ufahamu haukutayarishwa kupokea....swali kwako...mawazo mangapi mazuri,mapya yamekupita kwa sababu tu ulikosa udadisi juu ya jambo fulani?

3....hukufungulia ulimwengu mpya na yanayowezekana
Kwa kuwa mdadisi unapata fursa ya kuona ulimwengu mpya na kuvuka na kukutana na mambo ambayo ulidhani hayawezekani hapo awali...vitu vyote huwezi kuona kama si kwa udadisi.Hayo yamefichwa chini ya maisha ya kawaida (yasio ya udadisi)inahitaji udadisi kufunua na kugundua ulimwengu mwingine ambao hukuwahi kuwa kabla na kugunduka kuwa yanawezekana.
 
4...hufanya maisha kuwa na mvuto.
Maisha ya Udadisi ni tofauti sana na maisha ya kawaida yaliyodumaa na yanayojirudia.Maisha ya udadisi mara zote yana mambo mapya ambayo huvutia "attraction" na huwashika watu "attention".

Imeletwa kwenu na Mchungaji Matthew Sasali
www-aroma.blogspot.com

No comments:

Post a Comment