Friday, June 15, 2012

KOLO TOURE AVUTA JIKO.

BEKI wa kimataifa Ivory Coast na klabu ya Manchester City, Kolo Toure hatimaye amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi ambaye amezaa nae watoto wawili Chimene Akassou jijini Abidjan katika sherehe ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa kisiasa pamoja na wanamichezo wenzake. Toure alifunga harusi hiyo msikitini na shughuli hiyo inatarajiwa kuendelea Jumamosi ambapo wawili hao watasaini vyeti vyao vya ndoa kwa msajili na baada ya hapo sherehe kubwa imeandaliwa ambapo wachezaji wote wa timu ya taifa ya nchi hiyo wanatarajiwa kuhudhuria. Katika harusi hiyo ndugu yake Kolo ambaye wanacheza wote katika klabu ya Manchester City, Yaya Toure ndiye alikuwa msimamizi katika harusi hiyo ya kaka yake. Wawili hao wamekuwa wakiishi pamoja nchini Uingereza toka mwaka 2003 ukiwa ni mwaka mmoja toka Toure ahamie katika klabu ya Arsenal akitokea Asc Mimosas.

No comments:

Post a Comment