Monday, June 4, 2012

JAMHURI YA CZECH, UGIRIKI ZAWA TIMU ZA KWANZA KUWASILI POLAND.


 

TIMU za taifa za Jamhuri ya Czech na Ugiriki zimekuwa timu za kwanza kuwasili nchini Poland kwa ajili ya michuano ya Ulaya ikiwa imebakia wiki moja kabla ya kuanza kwa mechi za ufunguzi za michuano hiyo. Timu zote mbili zimepangwa kundi moja na wenyeji wenza Poland na Urusi katika kundi A ambapo wanatarajiwa kucheza mechi zao za ufunguzi Ijumaa ambapo Poland itacheza na Ugiriki ambao mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2004 jijini Warsaw wakati Urusi itacheza na Jamhuri ya Czech katika mji uliopo Kusini-Magharibi mwa nchi hiyo wa Wroclaw. Shirikisho la Soka la Ulaya limesema kuwa timu ya Jamhuri ya Czech iliwasili jijini Wroclaw ikitokea Prague kwa treni ya mwendo kasi ambayo injini yake ilikuwa imepambwa kwa rangi nyekundu, nyeupe na bluu ambayo inawakilisha rangi za timu hiyo. Timu ya Russia ambayo inanolewa na kocha Dick Advocaat iliwasili jijini Warsaw jana jioni wakitokea jijini Zurich, Switzerland walipokuwa wameweka kambi.

No comments:

Post a Comment