Tuesday, June 19, 2012

GYAN KUSAINI MKATABA WA KUDUMU, AL AIN.MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana, Asamoah Gyan anatarajia kusaini mkataba wa kudumu na klabu ya Al Ain ya Falme za Kiarabu-UAE. Gyan ambaye ana umri wa miaka 26 ameondoa uwezekano wa yeye kurejea Ulaya akisema kuwa ameyazoea mazingira pamoja na mfumo wa ligi wa UAE. Akizungumza akiwa nchini Ghana ambapo amekwenda kwa ajili ya mchezo wa hisani, mshambuliaji huyo amesema kuwa Al Ain wameonyesha nia ya kumsajili moja kwa moja na yeye pia angependa kubakia huko kwani hata familia yake nayo imeyapenda mazingira ya nchi hiyo. Mshambuliaji huyo ambaye amecheza msimu mzima uliopita kwa mkopo akitokea klabu ya Sunderland na kuibuka mfungaji bora wa ligi ya huko akifunga mabao 19 anatarajia kuongeza mkataba wake wa mkopo au wa moja kwa moja na klabu hiyo ili aweze kubakia. Kwasasa Gyan yuko nchini kwake kuisaidia Ghana kukusanya fedha katika mchezo wa hisani kati ya nyota wa timu ya taifa ya nchi hiyo na wasanii mchezo ambao utachezwa Jumapili jijini Accra.

No comments:

Post a Comment