Thursday, June 7, 2012

GLOBAL POLITICAL NEWS: CHINA IRAN LAO MOJA


Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba Iran na China zipo katika kambi moja ya kupigania amani, usalama na uadilifu duniani.
Ahmadinejad amesema hayo jana alipozungumza na Spika wa Bunge la China Wu Bangguo pambizoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Beijing. Aidha amesifu msimamo chanya na endelevu wa China katika kutetea haki zisizoweza kupingika za taifa la Iran katika taasisi za kimataifa hasa kadhia ya nyuklia ya Iran na kusema kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia inaunga mkono haki za taifa la China na itaendeleza mwenendo huo. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kuashiria kwamba mageuzi muhimu katika uga wa kimataifa yako njiani amesisitiza kuwa, ushirikiano wa Tehran na Beijing unaweza kufanya mabadiliko hayo yawe kwa manufaa ya mataifa na kwa ajili ya kuimarisha amani na usalama duniani na pia kuzuia kujipenyeza, kuingilia kati na kutumia mashinikizo wale ambao wenye lengo la kuzuia nchi nyingine zisisonge mbele. Kwa upande wake Wu Bangguo Spika wa Bunge la China amesema kuwa uhusiano wa Tehran na Beijing ni mzuri na kutaka kuimarishwa zaidi ushirikiano wa pande mbili katika nyanja zote.

No comments:

Post a Comment