Wednesday, June 13, 2012

GLOBAL NEWS: URUSI YAKANUSHA KUIUZIA SILAHA SYRIA

Urusi imekanusha shutuma za Marekani kwamba inaiuzia helikopta za kivita utawala wa Syria.
Akiwa ziarani nchini Iran, waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema silaha zote zinazouziwa Syria ni za madhumuni ya ulinzi na wala sio kutumiwa dhidi ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani. Lavrov ameishutumu Marekani kwa kuwapa silaha waasi nchini Syria, akisema Urusi inaipelekea Syria mifumo ya ulinzi dhidi ya mashambulio ya angani chini ya mkataba ambao haukiuki sheria za kimataifa. Wakati huo huo, serikali ya Syria imekanusha kauli ya Umoja wa Mataifa kwamba nchi hiyo imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, ikisema inapambana na magaidi.

No comments:

Post a Comment