Friday, June 15, 2012

GLOBAL NEWS: BENSOUDA KUANZA KAZI LEO ICC


Mwanamama kutoka Gambia Fatou Bensouda leo amechukua rasmi nafasi yake kama mwendesha mashitaka mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC.
 
Bensouda amedhamiria kuepuka shinikizo la mataifa ya magharibi la kuwakamata viongozi wa Afrika wanaotuhumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita. Bensouda mwenye umri wa miaka 50 amekuwa mwanamke na mwafrika wa kwanza kushika nafasi ya kuongoza jopo la kimataifa la waendesha mashitaka lenye makao yake mjini The Hague. Amefanya kazi kama msaidizi wa mwendesha mashitaka mkuu anayeondoka Luis Moreno Ocampo tangu mwaka 2004. Chini ya Uongozi wa Ocampo, raia wa Argentina, ICC imefungua mashitaka 25 yote kutoka nchi za Afrika.  

No comments:

Post a Comment