Saturday, June 16, 2012

GLOBAL BOXING NEWS: MRUSI AMKIMBIA MATUMLA


Bondia huyo wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana kama “Siberian Tiger” aliingia mitini kiaina baada ya kupelekewa tiketi za ndege ya shirika la Kirusi la Aeroflot yeye na kocha wake. Hii ni mara ya kwanza kwa mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika baada ya bondia mmojawapo kuingia mitini kwa woga.

Bondia Rashid Matumla anayejulikana kama Snake Boy ana rekodi ambayo mpaka sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia. Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki na Kati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani (WBU). Akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye kwa sasa ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa wa hali ya juu. Hata hivyo Rashid Matumla  amepangiwa kupigana na bondia mwingine siku za usoni  ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusi huyo!

Imetolewa na:
Onesmo A.M.Ngowi
President IBF/USBA for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
Director, BRAND-Africa
Coordinator, Moshi Sister Cities Committee
Coordinator, International Education & Resources Network (iEARN) to Tanzania

No comments:

Post a Comment