Friday, June 22, 2012

GEBRE SELLASSIE KUTUA WERDER BREMEN.

Theodor Gebre Selassie.
BEKI wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, Theodor Gebre Selassie amekubali kusaini mkataba na klabu ya Werder Bremen ya Ujerumani akitokea klabu ya Liberec ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Czech msimu uliopita. Wakati wa Gebre Selassie, Victor Kolar alithibitisha uhamisho huo leo ikiwa ni siku moja toka Czech waenguliwe katika michuano ya Ulaya nchini Poland na Ukraine baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Ureno kwenye hatua ya robo fainali. Klabu zote mbili zimeshakubaliana uhamisho huo na Bremem inatarajiwa kumpa mkataba wa miaka minne mchezaji huyo baada ya kufanyiwa vipimo vya afya nchini Ujerumani. Gebre Selassie mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akicheza katika kikosi cha kwanza katika timu ya taifa kuanzia mwaka jana ambapo aliisaidia timu hiyo kufuzu michuano hiyo na amekuwa mmoja wa wachezaji bora katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment