Sunday, June 24, 2012

EUSEBIO ALAZWA NCHINI POLAND.


 

MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Ureno, Eusebio amekimbizwa hospitali na kulazwa nchini Poland. Shirikisho la Soka la Ureno limesema kuwa Eusebio ambaye ana umri wa miaka 70 aliugua ghafla Jumamosi katika mji wa Opalenica ambapo amekwenda ili kuipa sapoti timu ya taifa ya nchini hiyo kwenye michuano ya Ulaya. Msemaji wa shirikisho hilo amesema kuwa nyota huyo wa zamani ambaye amewahi pia kukipiga katika klabu ya Benfica alipelekwa katika hispitali iliyopo jijini Poznan kwa ajili ya vipimo. Eusebio alikuwa nyota wa Ureno katika miaka ya 1960 na alitajwa kama mmoja wa wachezaji 10 bora wa waliowahi kutokea na Shirikisho la Soka Dunia-FIFA mwaka 1998.

No comments:

Post a Comment