Friday, June 22, 2012

EURO 2012 NEWS: HISPANIA Vs UFARANSA


B
aada ya juzi kushuhudia Ureno ikitinga hatua ya Nusu Fainali kwa kuitandika Jamhuri ya Czech bao 1 -0, Leo Ureno anamsubiri mshindi kati ya Hispania na Ufaransa. Pia Ujerumani naye anamsubiri atayeshinda katika mtanange kati ya Italia na England.

Mechi kati ya Hispania na Ufaransa inachezwa katika Uga wa Donbass Arena katika Jiji la Donetsk majira ya sa 3:45 kwa saa za Afrika mashariki.

Katika mechi hii ya leo kila timu itakuwa ikitafuta kumshinda mwenzake kutokana na rekodi za timu hizo kwenye michuano ya UEFA Euro kwani Ufaransa imetwaa Kombe hilo mara mbili na Uhispania mara mbili.

HISPANIA
Pia Uhispania itakuwa na kazi ngumu ya kulitetea taji hilo lisitwalie na timu nyingine pia Ufaransa ilishawahi kufika hatua kama hiyo ya kulitwaa na kisha kutwaa Kombe la Dunia hivyo leo ni shughuli pevu kwa kila timu kwani haijawahi kwa timu kutwaa mara tatu mfululizo.

La Fuja Roja (Hispania) wanaonekana kuendelea mbele kwa hatua  nyngine muhimu licha ya kwamba inakutana na timu ngumu ya  Les Blues ( Ufaransa) na kwamba Hispania wanaingia katika hatua ya Robo Fainali kwa ushindi mwembamba dhidi ya Croatia wa bao 1-0 na kukaa kilele mwa kundi C.

Endapo Hispania itapita katka hatua ya Robo na kutinga hatua ya Nusu Fainali basi itakosa huduma za wachezaji muhimu Xabi Alonso, Javier Martinez, Alvaro Arbeloa, na Joldi Alba na hapo huenda Vicente Del Bosque akamwacha Torres kama mshambuliaji ama la.

UFARANSA
Kwa upande wa Ufaransa walijikuta wakiwa katika hali mbaya baada ya kunyukwa na Sweden mabao 2-0 na kuipa nafasi England kukutana na Italia na kuongoza msimamo wa kundi C.

Ufaransa nao wataikosa huduma ya Mlinzi wa Klabu ya AC Milan Phillipe Mexes baada ya kuonyeshwa kadi ya njano ya pili siku walipocheza na Sweden na Laurent Koscielny atachukua nafasi yake.

Hata hivyo bado wana wasiwasi na “performance” ya Samir Nasri na Frank Ribery kutokana na kukosekana kwenye mazoezi siku ya Jumatano lakini wanategemea kuifanya mechi ya leo kuwa nzuri.

Yohan Cabaye hatakuwepo kutokana na majeruhi ya nyama ya paja ambayo itamfanya kukaa benchi aidha Jeremy Menez huenda akaanza leo licha ya kutolea katika mechi dhidi ya Sweden


Key Match Facts
1.      Hispania imepoteza mechi 2 kubwa katika michuano mikubwa tangu mwaka 2006 kwani alipoteza mechi yake dhidi ya U.S katika Conferedation Cup na Mechi ya Ufunguzi Kombe la Dunia 2010 dhidi ya Uswisi.
2.      Kwa juhudi ambazo zimefanyika sasa katika Euro 2012 Fernando Torres anabakia kuwa mfungaji pekee katika kikosi cha timu ya Hispania, amefunga mabao 30 katika mechi 96 alizocheza.
3.      Playemaker Xavi Hernandez amevunja rekodi ya Mdachi Ronaldo Koeman kwa kupiga pasi 127 katika mechi moja dhidi ya Jamhuri ya Ireland.
4.      Ufaransa imetunza rekodi ya kutopoteza michezo 23 mpaka mechi ya makundi alipopigwa na Sweden.
5.      Mabao ya Frank Ribery, Patrick Viera na Zinedine Zidane yalitosha kumuondoa Mhispania katika World Cup ya 2006 katika hatua ya 16.
6.      Mshambuliaji Karim Benzema ameshindwa kugusa nyavu katika mechi 4 zilizopita hasa ukizingatia kwamba alikuwa katika XI.

7.      Kocha Laurent Robert Blanc atakuwa ni kocha wa 5 wa taifa hilo ambaye ameichezea Timu  na baadaye kuwa Kocha. Aliichezea Ufaransa kuanzia mwaka 1989-2000 mechi 97 na kutupia kambani 16 pia amewahi kuichezea Klabu ya Man Utd kati ya mwaka 2001-2003 mechi 48 na kufunga goli 1
 Spain player to watch: David Silva.


France player to watch: Karim Benzema.

Spain
Casillas
Arbeloa,
Ramos,
Pique,
Alba
Busquets,
Alonso
Iniesta,
Xavi,
Silva
Torres

Ufaransa
Lloris
Debuchy,
Koscielny,
Rami,
Clichy
Cabaye,
M'Vila
Menez,
 Nasri,
Ribery
Benzema

Prediction: This Spain team is not of the vintage which won Euro 2008 and the 2010 World Cup, but few teams beset by in-fighting excel and Spain should win this without the need for extra-time or penalties.

No comments:

Post a Comment