Friday, June 22, 2012

EURO 2012 NEWS: EURO VIBE FANS ZONE, AJISHINDIA ZAWADI


M
shindi wa Zawadi katika EURO VIBE FANS ZONE amepatikana usiku wa kuamkia leo baada ya kushinda chemshabongo kuhusu mechi kati ya Ujerumani na Ugiriki ambayo imemalizika kwa Ujerumani kutinga Nusu Fainali ya Michuano hiyo barani Ulaya.

Mshindi wa Chemsha Bongo hiyo Erick Paul Bakilana mkazi wa Old Forest Jijini Mbeya amekabidhiwa zawadi yake na Programme Meneja wa Redio Mbeya FM kwa niaba ya Meneja wa Redio hiyo.

Bakilana ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ameusifu uongozi wa The Vibe Club na Redio Mbeya kwa kusema ni motisha kwa wasikilizaji wa Redio na wateja wa The Vibe Club.

Pia Bakilana amesema kujishindia jezi ya Ujerumani kumekuna zaidi kutokana na kwamba anaipenda timu ya Taifa ya Ujerumani na siku moja huenda akafika Ujerumani kutazama mechi moja ya timu ya taifa na kwamba siku moja ndoto hiyo itataimia tu.

Itakumbukwa kwamba katika Chemsha Bongo hiyo yalitolewa maswali yapatayo 7 kuhusu mechi hiyo ambayo Ujerumani imeendeleza rekodi ya kuinyuka kwa mechi ya 6 kati ya mara 9 walizocheza katika mashindano makubwa. 


 THE VIBE CLUB USIKU HUU
VIBE OUTDOOR MECHI IKIENDELEA
 MWANZONI KABISA MWA SHOW
 ERICK BAKILANA
 MENEJAWA VIBE CLUB RICHARD  AKIWA NA WAGENI WAKE WA MWISHO NIABDUL MAJID
 GWAMAKA GABRIEL MWANKOTA

 BAKILA AKIWA NA RAFIKI YAKE
 BAKILANA AKIPOKEA JEZI
 GWAMAKA MWANKOTA AKIKABIDHI
 BAKILA AKIONYESHA JEZI ALIYOSHINDA

No comments:

Post a Comment