Thursday, June 28, 2012

CORINTHIANS YAIDIDINDIA BOCA JUNIORS KATIKA FAINALI YA KWANZA COPA LIBERTADORES.

Romarinho.
KLABU ya Corinthians ya Brazil imefanikiwa kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Boca Juniors ya Argentina katika fainali ya kwanza ya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini iliyofanyika katika Uwanja wa La Bombonera. Alikuwa ni mchezaji wa Corinthians Romarinho ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba akichukua nafasi ya Danilo aliyeisawazishia bao timu yake hiyo katika dakika za lala salama za mchezo baada ya beki wa Boca Facundo Roncaglia kuifungia timu yake hiyo bao la kuongoza mapema katika kipindi cha pili. Boca ambao wanacheza fainali yao ya 10 katika michuano hiyo bado wanapewa nafasi ya kunyakuwa taji hilo kutokana na kuwa na rekodi nzuri ya kushinda michezo ya ugenini pindi anapokutana na timu za Brazil. Corinthians ambao wametinga fainali kwa mara ya kwanza bila ya kufungwa wanatarajia kutumia vyema mchezo wa fainali ya pili kuhakikisha wanalibakisha kombe hilo nyumbani ambao utachezwa nyumbani jijini Sao Paulo Jumatano ijayo.

No comments:

Post a Comment