Monday, June 4, 2012

BRAZIL YALALA 2-0 KWA MEXICO.

Javier Hernandez 'Chicharito'
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Mexico na klabu ya Manchester United, Javier Hernandez na kiungo wa anayecheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs, Gio Dos Santos jana waliisaidia timu yao taifa kuididimiza Brazil mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa katika Uwanja wa Dallas Cowboy nchini Marekani. Dos Santos ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 21 kabla ya Hernandez kufunga la pili kwa njia ya penati dakika 32 na kuipa ushindi Mexico mbele ya mashabiki 84,519 walioshuhudia mchezo huo. Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia walikuwa wanatumia mchezo huo kujaribu wachezaji wao vijana ambao watawatumia katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London wakati Mexico walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014 ambalo mwenyeji wake atakuwa Brazil. Brazil ikiwa na washambuliaji wake Neymar na Hulk ilishindwa kutamba mbele ya Mexico pamoja na kuifunga mabao 4-1 timu ya taifa ya Marekani kwenye mchezo ulichezwa Jumatano iliyopita.

No comments:

Post a Comment