Friday, June 22, 2012

BAROS ATUNDIKA DARUGA.

Milan Baros.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, Milan Baros ameamua kutundika daluga kuichezea timu taifa ya nchi yake baada ya kutolewa na Ureno kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya. Msemaji wa Shirikisho la Soka la Czech Jaroslav Kolar amesema kuwa Baros alitangaza nia yake hiyo katika vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya mchezo huo ambapo kila aliyekuwepo humo alimshukuru kwa kazi aliyoifanya katika kipindi cha miaka 11 aliyoitumikia klabu hiyo. Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 30 ambaye anakipiga katika klabu ya Galatasaray amefunga mabao 41 katika michezo 93 aliyocheza katika timu hiyo na kumfanya kuwa mchezaji wa pili kufunga mabo mengi zaidi katika nchi wa kwanza akiwa Jan Koller ambaye alifunga mabao 55. Katika michuano ya Ulaya mwaka huu hakufunga bao lakini alikuwa mfungaji bora katika michuano ya hiyo mwaka 2004 na pia akuwepo katika kikosi cha Liverpool kilichonyakuwa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment