Saturday, June 16, 2012

ASIA NEWS: MRITHI WA SAUDIA NAYEF BIN ABDUL-AZIZ AFARIKI DUNIA


Mahakama ya Kifalme ya Saudi Arabia, imetangaza kuwa mrithi wa kiti cha ufalme, Naif bin Abdul-Aziz, amefariki dunia hivi jana akiwa matibabuni nje ya nchi.

Mazishi ya kiongozi huyo mwenye miaka 78 yatafanyika kesho katika mji mtukufu wa Makka. Kituo cha habari chenye makao yake makuu mjini Dubai, al-Arabiyya, kimesema kwamba Naif amefariki katika hospitali moja nchini Uswisi. Naif aliteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha ufalme mwezi Oktoba mwaka jana, baada ya kifo cha kaka yake, Sultan. Mapema mwaka huu, Naif alikwenda nchini Marekani kwa kile kilichoitwa "uchunguzi wa matibabu". Alitumikia serikali ya nchi yake kama waziri wa mambo ya ndani tangu mwaka 1975 na akawa naibu wa pili wa waziri mkuu hapo mwaka 2009. Uteuzi wake wa kuwa mrithi wa ufalme ulizusha hofu miongoni mwa wapenda mageuzi nchini humo, wakisema kwamba angelizuia mageuzi yaliyoanzishwa na Mfalme Abdullah bin Abdul-Aziz.    

No comments:

Post a Comment