Friday, June 15, 2012

AFRICA NEWS: WAMISRI WANAPIGA KURA LEO


Wamisri wameanza kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa  nchi hiyo kati ya mgombea anayefuata  siasa zinazoegemea dini ya Kiislamu dhidi ya waziri mkuu  wa zamani wa utawala wa taifa hilo huku kukiwa na  hali ya wasiwasi na wakati  hali kisiasa baada ya mageuzi haieleweki.
Ahmed Shafiq, waziri mkuu wa mwisho wa rais alieondolewa madarakani Hosni Mubarak anapambana na mgombea wa chama cha Udugu wa Kiislam, Mohammed Mursi katika zoezi la kupiga kura litakalodumu kwa siku mbili ambapo kiasi ya raia milioni 50 wamejiandikisha kushiriki zoezi hilo. Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema asubuhi ambapo kiasi ya askari 150,000 wametawanywa kwa  nia  ya  kudhibiti hali ya usalama kwenye uchaguzi huo wenye mgawanyiko mkubwa. Kinyang'anyiro hicho kimeleta mtengano na hasa kwa wale wenye hofu ya kurejea madarakani kwa uongozi wa zamani kupitia Shafiq na wale wanaotaka kutenga siasa na dini na shaka kwamba  chama  cha Udugu wa Kiislamu kitavuruga uhuru wa watu. Katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo Mursi alipata asilimia 24.7 ambapo Shafiq ambae pia alikuwa kamanda wa jeshi la anga alipata  asilimia  23.6  ya kura.    

No comments:

Post a Comment