Monday, June 25, 2012

AFRICA NEWS: WAFANYAKAZI WA UN-WAGOMA


Wafanyakazi katika ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Entebe, Uganda wamefanya mgomo jana Jumatatu kulalamikia mazingira mabaya ya kufanyia kazi pamoja na kutaka nyongeza ya mishahara.

Wafanyakazi zaidi ya 120 walianza mgomo leo asubuhi na hivyo kukwamisha shughuli katika ofisi hiyo ya UN. Wafanyakazi hao wanasema kuwa Umoja wa Mataifa umeipa kampuni ya kibinafsi kandarasi ya kuendesha ofisi hiyo na kwamba kampuni hiyo sasa imekata mishahara yao kwa asilimia kubwa. Wameongeza kuwa hawana bima za afya wala barua za kuajiriwa na hivyo wanahisi kuwa UN inawafanya kuwa watumwa katika nchi yao. Wafanyakazi hao wamesisitiza kuwa hawatorudi kazini hadi pale mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Nchini Uganda atakapofika katika eneo hilo na kutatua matatizo yao.

No comments:

Post a Comment