Wednesday, June 20, 2012

AFRICA NEWS: HALI YA AFYA YA MUBARAK MAHUTUTI


Aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak, yuko katika hali mahututi hospitalini baada ya kupatwa na kiharusi. 
Hayo yalisemwa jana na wakili wake, Farid al-Deed,  katika taarifa iliyochapishwa leo na gazeti la Al Aharam nchini humo. Kauli hiyo inafuta taarifa zilizojitokeza awali kwamba Mubarak alikuwa amefariki dunia. Wakili huyo alisema jana hali ya kiongozi huyo wa zamani ilikuwa mbaya kutokana na ukosefu wa matibabu katika hospitali ya gereza lililo karibu na mji mkuu Cairo, ambako Mubarak alikuwa akitumikia kifungo cha maisha. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama, Mubarak mwenye umri wa miaka 84 alihamishiwa jana katika hospitali ya kijeshi katika kitongoji cha Maadi mjini Cairo. 

Taarifa kuhusu Mubarak zilijitokeza wakati maelfu ya watu walipokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Tahrir kupinga hatua ya baraza la kijeshi linaloitawala Misri, kujiongezea madaraka mapya.

No comments:

Post a Comment