Sunday, April 29, 2012

KILL ME PLEASE:PART ONE

TUNAENDELEA NA STORY YA KILL ME PLZ PALE ILIPOISHIA LAST SUNDAY
Hapo mwalimu likajitafutia mbinu ya kuwa karibu na Olga, likamuomba Olga apeleke vitabu vyake nyumbani kwake, binti wa wawatu bila kufikiria wala nn akakubali kwa heshima kubwa , alipofika nyumbani kwa mwalimu tu akalikuta hilo limwalimu limeshatangulia nyumbani ile olga kuingia ndani tu limwalimu likambaka msichana wa wa wa watu na kisha kumpiga mkwara kuwa akisema tu atamuua tena kwa mkono wake mwenyewe , mkwara huo ulimfanya Olga anyamaze na wala hakuwahi kumwambia mtu.....Bahati mbaya Olga kitendo cha kubakwa mara moja tu kwa vile hakuwa anajua mema wala mabaya akapata mimba..... na kama mnavyojua mimba hazijifichi mara moja akagunduliwa na kufukuzwa shule.... olga akarudi kwa mamaye akiwa mwenye masikitiko makubwa taabu na maisha ya pale kwao ni kitu kingine alichokuwa kikimuumiza sana but angefanya nini akajianzishia biashara yake ya kuuza mkaa somehow ndoto zake za kusoma zikazima kama vile nuru ya mshumaa inavyozima pale inapopulizwa na upepo......

Siku zilizidi kwenda hatimaye Olga alijifungua mtoto mzuri wa kiume aliyempa jina la Blessing..., japokuwa maisha yao yalikuwa ya shida but ujio wa mtoto somehow ulileta furaha fulani ndani ya nyumba , so wakarudi na kuwa watatu tena kama zamani, mtoto blessing aliendelea kukua vzr na akiwa mwenye afya njema, olga aliendelea na biashara ya kuuza mkaa na mamake akiuza mboga kwa kusaidiana waliweza kuishi maisha ya kawaida kabisa but still ya hali ya chini Baada ya miaka miwili mamake Olga alianza kuugua ugonjwa wa ajabu kila siku alikuwa akilalamika kuwa anaumwa na kichwa ,olga alimpeleka mamake hospital ili apate matibabu lkn mama alipata nafuu kidogo tu ila hakupona kabisa, akawa anaendelea kuumwa hivyohivyo tu , olga aliingiwa na uoga na akaapa kuwa hawezi kuacha mamake auugue hivyo coz hayuko tayari kumpoteza mamake no way mamake alihangaika naye sana so aliwaza kitu......

lazima nitafute kazi nitafute pesa ili niweze kumsaidia mama yangu, kwa bahati nzuri hapo kijijini kwao palikuwa na old friend ya mama yake alikuja kusalimia baada ya kuhamia jijini Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara na alipokuja salimia alisema ana rafiki yake tajiri mkubwa huko Mbeya anatafuta housegirl so kama kuna mtu yeyote angehitaji basi yy anaweza kwenda naye....Olga akajionea nafasi ndo hii wacha niende mjini nikatafute maisha so akamuaga mamake kwa masikitiko makubwa na kumwambia ucjali mom naenda kutafuta kazi ili nikusaidie uende hospital naomba wewe ukae na mwanangu mama naahidi mshahara wa kwanza tu nitawatumia wote ili muweze kupata mahitaji madogo madogo pamoja na pesa yako ya kwenda hospital

Kesho yake asubuhi na mapema Olga na yule mama wakaanza safari ya kwenda huko makao mapya, njiani alijiuliza maswali mengi ambayo hakuwa na majibu yake alijifikilia kwann anapata taabu zote anazozipitia ni wapi alikomkosea mungu hadi awaadhibu kwa taabu zote hizo na je ni nini hatima ya maisha yao, alianza kujifeel kuwa anamiss sana nyumbani ndani ya siku ile moja tu alimmis sana mwanae na akawa akimfikiria sana mamake ambaye alimuacha akiwa anaumwa huko nyumbani , anyway somehow alijikuta akijipa moyo kuwa huenda hivyo ni vipimo tu katika maisha na may b one day maisha yao yatabadilika na kuwa sawa na ya watu wengine Walifika Mbeya usiku wa maneno na wala hata hakuuona mji vizuri na moja kwa moja alipelekwa huko kwa boss mpya ambaye alikuta wamelala so alifunguliwa geti na walinzi naye akaonyeshwa sehemu ambayo alijitupia hivyo hivyo na tunguo twake tuchafu na kulala akiwa mchovu sana, then asubuhi alishtuliwa na maji ya bariiidi ambayo alimwagiwa na boss wake mwanamke na kuulizwa wewe hapa umekuja kufanya kazi au kulala! Alikurupuka na kujibu kwa sauti ya upole shikamooo mama, matherboss baada ya kujibu alisonya na kumrushia nguo na kumwambia hebu niondokee kaoge huko usije kuwaambukiza wanangu chawa!

 Olga alichukua hizo nguo na wala hakusema kitu akaenda kuoga na kubadirisha nguo kisha akaonyeshwa linyumba lote na makazi yote jinsi ya kufanya then akaingia kazini siku hiyohiyo , alifanyishwa makazi weee nusu aanguke klwa kizunguzungu lkn kila alipokuwa akikumbuka shida za nyumbani kwao wala hakujali alifanya kila kitu kwa moyo mmoja kabisaa alikaa kama siku tatu hv bila kumuona baba wa nyumba kumbe alikuwa amesafiri kwenda kusalimia wazazi wake alisafiri pamoja na wanae wawili wa kiume so siku ya nne baba mwenye nyumba alirudi na alipokuja alimchangamkia Olga vzr tu akamsalimu na bahati watoto wake nao walitokea kumpenda sana olga na walimuita dada so some how familia ikawa imepata mdada mzuri sana japo mama mwenye nyumba tu ndo alikuwa taabu.......... JE MAMA MWENYE NYUMBA NA OLGA HATIMA YAO NINI??? USIKOSE KUFATILIA STORY HII NEXT SUNDAY............ TO BE CONTINUED


MTUNZI-NYEMO DAVID.

No comments:

Post a Comment