Thursday, May 31, 2012

LIVERPOOL YAPATA MBADALA WA DALGLISH.

Brendan Rodgers akiwa na mwanae.
KLABU ya Liverpool ya Uingereza imefanikiwa kupata meneja mpya Brendan Rodgers ambaye amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu kwa ajili ya kukinoa kikosi cha timu hiyo. Rodgers alitangazwa ramsi kuwa mbadala wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Kenny Dalglish ikiwa umepita muda wa saa 24 baada ya kocha huyo kumpa taarifa mwenyekiti wa klabu ya Swansea, Huw Jenkins kuhusu nia yake ya kuondoka katika klabu hiyo. Kazi ya kwanza atakayokutana nayo Rodgers katika klabu hiyo ni kujaribu kumsajili kiungo wa kimataifa wa Iceland, Gylfi Sigurdsson kutoka klabu ya Hoffenheim ya Ujerumani kwa ada ya euro milioni 6.8 baada ya kushindwa kufikia makubaliano na klabu ya Swansea. Rodgers aliongea na maofisa wa Liverpool jana akiwemo mwenyekiti wa klabu hiyo Tom Warner baada ya Swansea kuikubalia klabu hiyo kufanya mazungumzo na kocha huyo ambaye ni raia wa Ireland ya Kaskazini. Katika taarifa yake Jenkins amethibitisha kufanya mazungumzo na Rodgers kuhusu nia yake hiyo na kwasasa wako katika mazungumzo na klabu ya Liverpool kuhusiana na suala hilo ambalo anategemea litaweza kumalizika katika kipindi cha saa 24 zijazo.

No comments:

Post a Comment