Tuesday, May 29, 2012

EURO 2012: HODGSON ATAJA KIKOSI CHA MWISHO.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ambao wataiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Ulaya linalotarajiwa kuanza mapema mwakani. Katika kikosi hicho ambacho hakina mabadiliko makubwa na kile alichotangaza mara ya kwanza Hodgson amewajumuisha Danny Welbeck na Glen Johnson ambao walikosa mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo na Norway kutokana na majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua. Mabadiliko yaliyopo katika kikosi hicho ni kuitwa kwa beki wa Everton Phil Jagielka kuja kuziba nafasi ya Gareth Barry ambaye aliumia nyonga wakati wa mchezo dhidi ya Norway ambao Uingereza ilishinda bao 1-0 jijini Oslo. Barry ambaye amecheza mechi 50 katika kikosi hicho cha Uingereza alizimika kutolewa nje ikiwa ni dakika 30 toka alipoingia kama mchezaji wa akiba katika muda wa mapumziko wa mchezo huo. 

KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: 1. Joe Hart (Manchester City), 13. Robert Green (West Ham), 23. Jack Butland (Birmingham City). MABEKI: 12. Leighton Baines (Everton), 5. Gary Cahill (Chelsea), 3. Ashley Cole (Chelsea), 2. Glen Johnson (Liverpool), 14. Phil Jones (Manchester United), 15. Joleon Lescott (Manchester City), 6. John Terry (Chelsea), 18. Phil Jagielka (Everton). VIUNGO: 19. Stewart Downing (Liverpool), 4. Steven Gerrard (Liverpool), 8. Frank Lampard (Chelsea), 16. James Milner (Manchester City), 20. Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), 17. Scott Parker (Tottenham), 7. Theo Walcott (Arsenal), 11. Ashley Young (Manchester United). WASHAMBULIAJI: 9. Andy Carroll (Liverpool), 21. Jermain Defoe (Tottenham), 10. Wayne Rooney (Manchester United), 22. Danny Welbeck (Manchester United).

No comments:

Post a Comment