Kocha wa kikosi hicho Cesare prandelli alimuacha mshambuliaji huyo ambaye anacheza klabu ya Manchester City katika kikosi hicho kutokana na matukio yake ya kushindwa kudhibiti hasira zake lakini Balotelli aliomba radhi na kocha huyo kumjumuisha katika kikosi chake tena. Mapema wiki hii Balotelli alinukuliwa na vyombo vya habari akionya suala la ubaguzi wa rangi katika michuano ya Ulaya ambayo itafanyika nchini Poland na Ukraine kwamba shabiki yeyote atakayemfanyia hivyo basi hatasita kumuua na yeye kwenda jela. Italia imepangwa katika kundi C kwenye michuano hiyo pamoja na timu za Hispania, Croatia na Jamhuri ya Ireland.
Thursday, May 31, 2012
BALOTELLI NDANI YA SUTI.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Italia Mario Balotelli ameonyesha kwamba anaweza kuvaa mavazi ya heshima akiamua kutokana na kuzoeleka na mavazi ya vijana katika maeneo mengi ambayo amekuwa akitembea anapokuwa nje ya uwanja. Tukio hilo lilitokea wakati mchezaji huyo pamoja na kikosi kizima cha timu ya taifa ya nchi hiyo walipopiga picha ya pamoja kwa ajili ya michuano ya Ulaya 2012 wakiwa wamevalia suti nyeusi kitendo ambacho hakijazoeleka kwa mchezaji huyo mwenye vituko vingi ndani na nje ya uwanja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment