Wednesday, May 30, 2012
"ALL IN ONE RHYTHM" NEW SLOGAN FOR BRAZIL 2014.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza kauli mbiu inayoitwa Sauti Moja kwa Wote au kwa lugha ya kigeni All in one rhythm itakayotumika katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014. Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke amesema kuwa kazi ya kutafuta kauli mbiu hiyo ambayo inawakilisha ladha tofauti imefanywa kwa pamoja kati ya serikali ya Brazil na shirikisho hilo na kutangazwa rasmi kwenye sherehe zilizofanyika jijini Rio de Jenairo. Naye Waziri wa Michezo wan chi hiyo, Aldo Rebelo amesema kuwa kauli mbiu hiyo ni mwaliko wa wenyeji na wageni ambao watakuja Brazil kuungana pamoja na kushangilia michuano hiyo ya kihistoria. Hiyo ni safari ya kwanza ya Valcke kwenda nchini Brazil toka alipokwaruzana na serikali ya nchi hiyo Machi mwaka huu kuhusiana na maandalizi ya michuano hiyo kitendo ambacho yeye na rais wa FIFA Sepp Blatter waliomba radhi. Serikali ya Brazil ilipanga kutumia kiasi cha dola bilioni 13 katika miradi 101 ya kujenga na kukarabati viwanja, kukarabati viwanja vya ndege, barabara na usafiri wa jumuia lakini ni miradi 60 kati ya hiyo ndio imeanza mpka sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment