Saturday, January 21, 2012

Weekend ndio hii imefika. Week nzima umeitumia kufanya kazi, na weekend ndio muda mzuri wa kuspend na familia yako. Wewe utaspend vipi weekend yako?

                  Watoto wakiwa sehemu za kuchezea, hii ni moja ya sehemu unaweza kwenda na mwanao
                                    Hii ni Tanzania yetu, wala si ulaya. Siku moja moja si mbaya
      Ukiwa nje ya nchi, siku za sikukuu au weekend, utaona wazazi, wakiwa na watoto wao, wakitembea sehemu mbalimbali, madukani, sehemu za michezo..ili mradi familia ipo pamoja.
      Ila kwa Tanzania yetu, mara chache utakuta wazazi wametoka na watoto wao, baba atatoka peke yake, au zaidi atatoka na mkewe.
      Hebu wazazi tujitahidi weekend moja, baba na mama, tuende sehemu, na watoto wetu. Vitu kama hivi hujenga uhusiano mzuri ndani ya familia.
     Angalau  4hours mkae na watoto,katika mazingira ya tofauti na nyumbani then usiku wazazi muende mnakotaka, kama bar, mziki etc..siku hizi Bongo yetu imeendelea banaa..sehemu nyingi tulivu za kukaa kifamilia.Watoto nao wanastahili kutoka, na kufurahi mazingira tofauti na nyumbani.

No comments:

Post a Comment