Saturday, January 21, 2012

Long distance Love Is Killing Me jamani....Naombeni ushauri wenu


Mimi ni msichana, nina umri wa miaka 26, nina boyfriend, na tumeshatambulishana kwa wazazi. Mimi niko nje kimasomo, boyfriend yuko Tanzania. Ila kila mwaka summer hua naenda nyumbani kusalimia. Tatizo langu ni hili, nikiwepo nyumbani Tanzania, mwanaume anakua ananijali, ananiheshimu. Yaani nakua na furaha na amani. Ila nikisharudi shule tu, anaanza vituko, mara yuko na wanawake wengine. Wanawake zake wananitafuta na kunitukana, tunakua kila siku ni ugomvi na hamna amani. Na nikifikia uamuzi wa kumuacha, ananiomba msamaha, anasema anafanya yote hayo kwa sababu niko mbali. Na anasema hawezi kupeleka msichana mwingine kwao, kwa sababu wananijua tayari, na wananipenda sana. Na anasema yeye anaamini future yake iko na mimi tu. Mtu wa hivi nimueleweje jamani?ananipenda kweli? 

No comments:

Post a Comment