Friday, March 30, 2012

Je wajua viungo vya chakula vinavyosaidia kupunguza mwili?

1. Mdalasini
   Harufu ya mdalasini humfanya mtu asijisikie hamu ya kula, pia hudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu hivyo kuzuia mkusanyiko wa mafuta mwilini. Ongeza mdalasini kwenye kawaha, chai, asali.
 2.Iliki
Iliki  ina chembechembe zinazozuia mkusanyiko wa mafuta kwenye mwili.Unaweza kuitumia Iliki kwenye chai, maziwa, kahawa. 
  3. Jeera ( Cumin)
   Zamani Ugiriki walikua wanawapa wanariadha wao Jeera kabla ya mashindano ili wasisikie njaa kuepuka kuwapa chakula kabla ya mashindano na kuwajaza matumbo kabla ya michuano.Itumie Jeera kila unapojisikia njaa itakufanya ujihisi umeshiba. Mbali na hayo ina ladha nzuri na huleta harufu nzuri kinywani. 

  4. Pilipili Mtama(Black Pepper)
  Ina uwezi wa kuua seli zenye mafuta mwilini.Pia inasaidia sana kupunguza kiungulia.
 5.  Manjano.
 Manjano inasaidia sana kwenye digestion ya chakula. Pia inauwezo wa kuzuia cell kujikusanya na kutengeneza mafuta mwilini.

   6.  PiliPili Kichaa 
Pilipili inauwezo wa kufanya mwili kudigest chakula haraka.
 7.Tangawizi
Tangawizi huongeza joto mwilini, kwa hiyo kuharakisha  metabolic processes mwilini.

Inawezekana ulikua unatumia tu, bila ya kujua kua viungo hivi vina manufaa mengine zaidi ya kuongeza ladha kwenye chakula. Niameanzaje sasa kuvitumia kwa fujo mie...xoxoxooo

No comments:

Post a Comment