Monday, June 4, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: DC AWANIA UONGOZI YANGA


MKUU wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu pamoja na mwanachama wa klabu ya Yanga Abdallah Binkleb juzi wamechukua fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe katika uchaguzi wa klabu ya Yanga uliopangwa kufanyika Julai 15. 

Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga  Francis Kaswahili amesema wanachama hao wanafanya idadi ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafsi mbalimbali za uongozi katika klabu hiyo kufikia  10 .

Mbali na hao wanachama wengine waliochukua fomu ni pamoja na John Jambele anayewania uenyekiti, huku Ayoub Nyenzi akiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti. 

“Waliochukua fomu kuwania ujumbe wa kamati ya Utendaji mbali na Muhingo na Binkleb  ni  Isack Chandi, Jumanne Mwamwenye na Salehe Hassan,”alisema.

No comments:

Post a Comment