Kampuni ya Kitwe General Trading ya jijini Dar-Es-Salaam inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bwana Lucas Rutainurwa imelitunuku cheti cha heshima Shirilisko la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA).
Daryl Peoples na Onesmo Ngowi
Sherehe za kukabidhi chezi hicho zilifanyika katika jiji la Honolulu, Hawaii nchini Marekani na Kitwe iliwakilishwa na Rais wa Shirikisho la IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti hicho kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kitwe General Trading, Rais Ngowi alisema kwamba IBF/USBA imetunukiwa kwa juhudi zake za kuendeleza mchezo wa ngumi katika bara la Afrika ambazo zinachangia sana katika kukuza ajira na biashara ya Utalii. Naye Rais wa IBF/USBA duniani Daryl Peoples wa Marekani alimshukuru sana bwana Rutainurwa kwa juhudi zake za kuendeleza mchezo wa ngumi Tanzania. Peoples aliahidi kwamba atamsaidia bwana Rutainurwa ili kuifanya Tanzania iwe ni Las Vegas ya ngumi katika bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment